Tuesday, August 2, 2011

MRATIBU NA AFISA AFISA HABARI WA ANTI-SLAVERY KUTOKA NCHINI UINGEREZA WATEMBELEA SHIRIKA LA KIVULINI KUJIONEA MIRADI INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA LAO


Mwenyekiti wa watoto wafanyakazi wa nyumbani, Angela Benedictor akimweleza Mratibu wa Mradi wa wafanyakazi wa nyumbani kutoka Anti-Slavery Bi.Audrey Guichon kuhusu miradi inayoendeshwa kwa ufadhili wao walipotembelea ofisi za kikundi cha Wote Sawa, Kivulini Mwanza.


Mratibu wa Mradi wa wafanyakazi wa nyumbani Bi. Audrey Guichon (katikati) akimweleza jambo Afisa habari wake Bw. Paul Donohoe kwenye ofisi za wote sawa, Kivulini.


Watoto wafanyakazi wa nyumbani wakifurahi pamoja na wageni wao walipowatembelea katika mradi wao wa kushona nguo kwenye kikundi cha Wote Sawa.


Bi. Audrey Guichon na Bw. Paul Donohoe wakitambulishwa kwa wafanyakazi wa nyumbani wanaopatiwa mafunzo ya kompyuta pamoja na staff wa Kivulini.

Bi. Audrey Guichon na Bw. Paul Donohoe wakifuatilia utambulisho


 Baadhi ya staff wa Kivulini wakiwasikiliza wageni wao.





No comments:

Post a Comment