Wednesday, July 13, 2011

VIKUNDI 8 KATIKA MASHINDANO YA KWAYA NA NGOMA ZA ASILI-GEITA.



Wasanii wa kikundi cha ngoma Buligi wakionyesha 
umahiri wa kucheza ngoma ya kabila la Wasukuma

Kaseni Traditional Dance wakijimwaga
na ngoma ya Kijita.



Kwaya ya Chanika wakijimwaga na wimbo wa 
kupinga ukatili majumbani

Kwaya ya Nyamigana


Majaji wakiwajibika kumpata mshindi
Kwaya ya Senga ikitumbuiza


Buhangiza Mlamani Kwaya na wimbo wa kupinga
ukatili dhidi ya makundi maalumu


Kwaya ya Chanika wakiimba wimbo wa
kushukuru Shirika la Kivulini.


Buligi nao hawakuwa nyuma, waliitaka jamii kubadilika 

Bi.Leah Soteli akiwapongeza washiriki

Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw. Philimon Shelutete 
aliwakilishwa na katibu tarafa Bw.Maungo (Kulia kwake ni Bi.Leah Soteli na Afisa Maendeleo wa kata Bw. Lucas Kidakawa.


Kikundi cha wanamabadiliko cha Tunaweza Chaniza Tubadilike (TCT) kimefanya mashindano ya kwaya na ngoma za asili July 10,2011 katika kijiji cha Kaseni kata ya Senga, Tarafa ya Bugando-wilayani Geita ili kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia sanaa.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Williamu Manyama alisema kuwa dhamira yao ni kuona jamii inaishi katika familia salama zisizo na unyanyasaji hivyo kuepukana na gharama za matibabu, ulemavu, vifo, uhasama, umaskini, kuvunjika kwa ndoa na ongezeko la watoto wa mitaani.

Alisema kuwa kupitia kampeni ya TUNAWEZA "We Can" kikundi chao kimefanikiwa kusuluhisha ndoa 10 zilizokuwa hatarini kuvunjika na kusajili jumla ya wanamadiliko 4,850 katika vijiji nane ndani ya kata mbili za Senga na Kagu ambapo lengo ni kuifikia wilaya nzima ya Geita.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Bi.Veneranda Kaluletela pamoja na kulishuru shirika la Kivulini alibainisha kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wananchi kuwaunga mkono kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, wasichana na watoto.

Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Philimon Shelutete mbali na kupongeza jitihada zinazofanywa na kikundi hicho aliahidi ofisi yake kuwapa msaada wa hali na mali katika kufikia malengo yao.
                                               

No comments:

Post a Comment