Thursday, September 29, 2011

ZAIDI YA WASHIRIKI 15 KUTOKA SHIRIKA LA KIVULINI WAUDHURIA TAMASHA LA 10 LA JINSIA TANZANIA

Mkurugenzi wa mtandao wa jinsia (TGNP) Bi.Usu Malya akimkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi tamasha hilo katika viwanja vya TGNP Mabibo, Dar es Salaam .
Baadhi ya washiriki kutoka shirika la kivulini (kutoka kushota) ni Afisa utawala Bi Martina Mashaka, Daktari Sheba na Mkurugenzi wa shirika hilo Bi Maimuna Kanyamala.




Amina Kisero (wa pili kulia) akiwa na zawadi ya kikoi baada ya kufunika kwenye workshop ya wanawake viongozi katika tamasha hilo.
Mwanaharakati Masesa Bandoma kutoka Kivulini akizungumza kwa hisia kali katika tamasha hilo

Mwanaharakati wa kabila la Kimasai kutoka Loliondo akizungumzia mgogoro wa Ardhi baina yao na mwekezaji.
Wanaharakati wa Tunaweza nao walitumia fursa hiyo kusajili wana mabadiliko
Edzen wa Kiss FM (Katikati) akiwa na ma-redio presenterz wenzake wakiwakilisha Tunaweza Kampeni.
Banda la watoto wafanyakazi wa nyumbani (Kivulini) lilikuwa kivutio kwa watu mbalimbali wakiwemo watoto wa shule

Mama Cash (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Wote Sawa, Angel Benedictor (kulia) alipotembelea banda la watoto wafanyakazi wa nyumbani. Katikati ni Mkurugenzi wa Kivulini Bi. Maimuna na Afisa Utawala Mama Mashaka.
Wasanii wa Ngoma na sarakasi wa Mjomba band wakionyesha manjonjo katika tamasha hilo.
Mrisho Mpoto (Mjomba) naye hakuwa nyuma
Kundi la wasanii wasioona nao walikuwa kivutio katika uimbaji wa mashahiri.
Wapenzi wa jinsia moja (MASHOGA) nao walikuwepo
Mashoga wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika tamasha kabla ya kuibuka na madai ya kutambuliwa katika katiba mpya.